Msemaji wa timu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire amedai kuwa timu ya Simba itafungwa magoli mengi leo itakapocheza nao huku Mwanza katika mchezo wa mzunguko wa pili baada ya kushinda mchezo wa raundi ya kwanza.

Akizungumza na wanahabari, Bwire alieleza kuwa mashabiki waje wengi uwanjani kushuhudia msimbazi wakichinjwa waziwazi.

Yaliyosemwa, “Mashabiki waje uwanjani wasisimuliwe wala wasikae kuangalia kwenye TV, kama wanauwezo wa kufika Kirumba wafike waone kwa macho yao nini vijana wetu watafanya dhidi ya Simba. Simba benchi lao la ufundi linaongozwa na kocha wa kigeni, pia wana wachezaji wengi wa wa kigeni lakini sisi tuna vijana watanzania wote.

Tunataka kuonesha vijana wa Tanzania wanauwezo wa kucheza ila hawathaminiwi lakini ili ubora wao uonekane ni kuwahudumia vizuri.

Simba wanaojinadi wapo level nyingine sisi tunataka kuonesha tupo level nyingine zaidi yao. Kaizer Chiefs wanatutazama na nina hakika watatukubali kwamba sisi ni zaidi ya Simba iliyowafunga gali 3-0 kwa Mkapa. Nina uhakika Kaizer Chiefs watatutafuta kutupongeza”, alieleza Bwire.

Simba inaendelea kucheza mechi zake katika kujihakikishia kubeba kombe la VPL kwa mara ya nne mfulululizo. Je, Bwire atafanikisha kweli kuwalaza na viatu wanamsimbazi? au yatakuwa ni maneno ya msemaji tu?


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa