Carlinhos Avunja Mkataba Yanga

Mchezaji kiungo wa Yanga, Carlinhos Harmo amevunja mkataba na timu yake ya Yanga baada ya kile kinachodaiwa kuwa ni matatizo ya kifamilia huko nyumbani kwao Angola.

Taarifa rasmi zinadai kuwa Carlinhos amewahi kutaka kuvunja mkataba na Yanga kwa mara mbili nyuma, baada ya majaribio ya mwanzo kufeli. Mara ya kwanza Carlinhos alijaribu kufanya hivyo kutokana na kudai kuwa anakaa mbali na mkewe na Yanga wakamleta mke wake.

Mara ya pili ilikuwa pale ambapo Carlinhos alitaka kupata huduma tofauti na wachezaji wa Yanga kutokana na ubora wake, Yanga nao wakaendelea kumsaidia ila katika hii mara ya mwisho ni pale ambapo mke wake alienda kujifungua kwao Angola.

Carlos akaanza kuleta tamthilia nyingi akikataa kucheza mechi nyingi kwa madai kuwa na majeraha mengi. Hizi ni rekodi za muangola huyu toka ajiunge na Yanga.

🔹Asisti: 3
🔹Mabao: 3
🔹Mechi: 9

Hatimaye, Uongozi wa Yanga ukaridhia kuvunja mkataba kwa makubaliano. Kama Atapata Timu Tanzania, Carlinhos atatakiwa kuilipa Yanga kiasi cha dola 200,000 (Zaidi ya Tsh Mil 450).

Inadaiwa pia makubaliano mengine ya kuvunja mkataba ni kuwa kama Carlinhos atapata timu nje ya Tanzania, atatakiwa kuilipa klabu robo tatu ya ‘signing fees’ aliyochukua.
Mchambuzi wa soka Tanzania Ali kamwe ametoa maoni yake kama isomekavyo,

“Kwa kuthamini kipaji cha Carlinhos, Uongozi wa Yanga ulifanya kila kitu kwa ajili ya kuhakikisha anacheza soka katika mazingira mazuri hapa Tanzania

Lakini moyo wa Carmo ulishaingia kiza. Hakutana kuendelea kubaki Yanga. Alifanya kila kitu kuondoka. Ni nafasi sasa kwa uongozi wa Yanga Kujifunza jambo katika USAJILI WAO unaokuja.

Wanatakiwa kufanya tafiti ya kutosha ya kiufundi, kinidhamu, kimazingira na tamaduni kwa wachezaji wanaowatoa kutoka nje ya Tanzania. Carmo sio wa kwanza wala hatakuwa wa mwisho.

Wako wachezaji/makocha wengi duniani wamewahi kuathirika na mazingira/tamaduni za mataifa wanayokwenda kucheza/kufundisha nje ya kwao. Wanachotakiwa kufanya viongozi wa Yanga kujiridhisha katika maeneo mengi mbali na kuomba tu ‘Clip za YouTube’ kutoka kwa Mawakala wa wachezaji”.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe