Ilikuwa Jumamosi mwanana kabisa, nchi ya Tanzania pamoja na zile jirani zilikuwa zikisubiria derby ya Kariakoo, mechi ya watani wa jadi, Simba vs Yanga. Uzito wa mechi kati ya timu hizi huvuta na kuteka hisia za watu wengi sana sio ndani tu, na nje ya nchi kabisa.

Nyoyo za mashabiki wa pande zote mbili zilikuwa na bashasha za kutaka kujua hatima ya mchezo huo. Ndimi za hawa mashabiki sasa! Ewala maneno mengi ya tambo na majivuni yaliendelea bila kujua makubwa yanayoweza kufikwa.

Ilipofika majira ya saa nane mchana, taarifa ilitolewa na shirikisho la soka Tanzania, TFF, kwamba wamepokea taarifa kutoka wizara ya habari, mawasiliano na michezo kuwa mchezo huo usogezwe mbele kutoka saa 11.00 jioni mpaka saa 1.00 usiku.

Katika barua hiyo hakukuwa na maelezo yoyote kuhusu sababu ya derby hiyo kusogezwa mbele, lakini licha ya taarifa hiyo kufikishwa timu zote mbili, Yanga walitoa taarifa kwa umma kwamba wanapinga uamuzi huo na kuamua kutokea kwenye mechi katika muda wa awali uliopangwa licha ya kutokuwa na mwamuzi yeyote wa mchezo.

Mwisho wa siku Yanga wanafanya mazoezi kabla ya derby kuanza na wanaingia uwanjani wanakaa kwa dakika kadhaa kisha wanatoka nje ya uwanja na kuondoka. Upande wa pili Simba wanaingia kwa muda wa taarifa ya pili na kuamua kufika uwanjani kwa muda wa saa 1.00 jioni lakini wanapigwa na butwaa kuhusu yanayoendelea.

Mpaka sasa hakuna taarifa zozote kutoka  mamlaka tajwa, wizara ya michezo, TFF wala bodi ya ligi ambayo imetoa maelezo yoyote kuhusu mustakabali wa derby hii ambayo inatazamwa na watu wengi Afrika kwa sasa. Uhairishwaji holela wa mechi hii umeleta madhara mengi kwa mashabiki, wadau wa soka, na hata taswira nzima ya soka la Tanzania huko nje za nchi.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

derby, Derby Ya Kariakoo Yatetemeshwa!!!!, Meridianbet

SOMA ZAIDI

8 MAONI

  1. Nyoyo za mashabiki wa pande zote mbili zilikuwa na bashasha za kutaka kujua hatima ya mchezo huo. Ndimi za hawa mashabiki sasa! Ewala maneno mengi ya tambo na majivuni yaliendelea bila kujua makubwa yanayoweza kufikwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa