Mshambuliaji namba moja ndani ya Azam FC, Prince Dube amesema  kuwa leo watapambana kupata ushindi mbele ya Rhino Rangers kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Mchezo wa leo utachezwa majira ya saa 10:00 jioni ikiwa ni hatua ya robo fainali na mshindi wa mchezo atapambana na mshindi wa mchezo kati ya Simba na Dodoma Jiji ambao nao pia utachezwa leo saa 1:00, usiku Uwanja wa Mkapa.

Dube mwenye mabao 14 ndani ya ligi akiwa ni namba moja kwa utupiaji amesema kuwa wapo tayari kupata matokeo leo na watafanya kwa ajili ya timu.

Dube - azam“Kwa ajili ya timu yetu tutapambana ili kupata matokeo tunajua kwamba mashabiki wanahitaji matokeo nasi pia tutafanya hivyo.

“Kikubwa ni kwamba maandalizi yapo sawa na kila kitu kinakwenda vuzuri hatuna mashaka licha ya kwamba tunajua kwamba tutapata ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wetu,“.

Ni Uwanja wa Kambarage, Shinyanga mchezo huu utachezwa ili kupata mshindi ndani ya dakika 90.


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa