Ndondo Cup 2021 kuanza Kutimua Vumbi Leo

Mashindano yanayohusisha timu za mtaani, Ndondo Cup inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo, huko shekilango.

Mwanzilishi na mfadhili wa mashindano hayo Shaffih Dauda ameeleza hayo katika taarifa yake kwa umma.

“Leo Jumapili Mei 23, 2021 tunaukata UTEPE wa michuano ya Ndondo Cup ikiwa ni msimu wa nane! Mechi ya ufunguzi itaikutanisha MANZESE UNITED 🆚 MAKUBURI FC, mechi itaanza saa 10:00 kwenye uwanja wa KINESI, SHEKILANGO.

Kuna mengi mazuri makubwa na ya tofauti kwa msimu huu kwenye Ndondo Cup, utofauti wa msimu huu upo kwenye maeneo yafuatayo.

MSHINDANO MATATU YA VIJANA

Wakati tunaanza na Ndondo Cup Academy lengo kubwa lilikuwa kuwa na Mashindano matatu ya vijana, mwaka huu kwa mara ya kwanza tutakuwa na mashindao ya U15, U17 na U19.

NDONDO CUP WANAWAKE

Kutakuwa na Ndondo Cup kwa soka la Wanawake kwa sababu ukiangalia mamlaka zote za za soka kuanzia FIFA, CAF na TFF soka la wanawake ni kipaumbele.

Sisi kama wadau wa mpira tumeliona hilo na kulibeba ili kuunga mkono juhudi za TFF na DRFA ili kufikia malengo kwenye kuendeleza mpira wa miguu wa Wanawake Tanzania.

ZAWADI

Wakati tunaanza mwaka wa kwanza Bingwa alichukua Tsh. Mil 3,000,000 leo ni mwaka wa nane, Bingwa atachukua Tsh. Mil 20,000,000.

NB: Hizi ni mechi za awali, [hatua za mwanzo] ambapo zipo timu 46 zilizogawanywa kwenye makundi nane. Kila kundi linatoa timu mbili halafu kuna kundi litatoa timu tatu.

Timu 16 zilizofika hatua ya 16 bora msimu uliopita zenyewe zimejihakikishia kucheza hatua ya makundi, lakini kati ya timu hizo, timu tatu hazijathibitisha ushiriki wao msimu huu maana yake kuna nafasi tatu zipo wazi.

Kwa hiyo msimu huu timu 19 zitafuzu kutoka hatua ya awali kwenda kuungana na timu 13 kwa ajili ya hatua ya makundi”, aliandika Shaffih Dauda.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

3 Komentara

    Mtanange wa kibabe

    Jibu

    Pambano la nguvu

    Jibu

    Patachimbika

    Jibu

Acha ujumbe