Beki wa kati wa timu ya Yanga, Abdallah Shaibu maarufu kama “Ninja” amepania kuchukua namba ya mabeki wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo, Bakari Mwamnyeto na Lamine Moro.
Suala liliwekwa wazi jana kati mechi ya viwango vya juu kabisa kati ya Yanga dhidi ya Azam, Ninja alikuwa na wakati na kiwango kizuri sana hapo jana licha ya timu yake kupoteza mechi hiyo.
Katika mechi ya jana, kulikuwa na vita kubwa sana kati ya Abdallah Shaibu na mshambuliaji wa Azam, Prince Dube ambaye ndiye aliyefunga goli la kuamua mechi kwa upande wa Azam. Ninja alionekana kufika kwa wakati kwenye matukio na kufanya safu ya ushambuliaji wa timu ya Azam kupata wakati mgumu sana.
Ndani ya mechi hiyo pia, ilionekana kama Dickson Job, pacha wa Abdallah Shaibu hakuwa kwenye wakati mzuri sana na kumfanya Ninja aonekane kama anacheza namba mbili, 4 na 5. Huu ulikuwa mchezo wa kwanza wa kocha mpya wa Yanga An Nabi, naamini ana mengi ya kujifunza kutoka kwenye mechi hii.
Toka arejee kutoka kucheza soka la kulipwa kule Marekani Ninja amekuwa akikosa namba katika kikosi cha kwanza cha timu ya wananchi lakini baada ya mabeki wa kati wa timu hiyo, Lamine Moro na Mwamnyeto kuwa na majeraha, Abdallah Shaibu amefanikiwa kuonesha kiwango cha juu sana pengine hata kuwazidi wategemezi hao wa Yanga.
Kutokana na mchezo wa jana na michezo kadhaa ya nyuma, kiukweli walinzi wa Yanga, watakuwa na kazi kubwa sana kurudi kwenye nafasi zao hasa kwa ujio huu wa kocha mpya.
Matokeo hayo ya jana yanaendelea kuwafanya Msimbazi kusali kileleni wakiwa na alama 58 na michezo mitatu mkononi, huku Yanga na Azam zikibaki nafasi zao zilezile huku “gap” la Yanga na Azam likiendelea kupungua wakipishana kwa alama 3 tu lakini Yanga wana mchezo mmoja nyuma ya Azam.
Kwani Meridianbet Wanasemaje! Mkwanja Upo Kwenye Kasino mpya ya Mini Power Roulette.
Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?
warda
Ataipata tu akaze buti
Elika
Sasa si wampe
Sania mapua
Penye nia pana njia
Magdalena
Kila la kheri
Adelta
Wampe tu
dorophina
Kila lakheri kama atafanikiwa
Issa
Bek bora kutokea
Venerose
Juhudi zake ndizo zitakazo mfikisha anapotaka
Lydia Emmanuel Magoti
Wampe tuuu
aisha
ajitahidi atapata
Sarah
Waampe tu