Rasmi Simba Bingwa VPL 2020/2021

Baada ya papatu


papatu ya dakika tisini za kushambuliana kwa wakati huku Simba wakionekana wapo kwenye wakati mzuri, ni rasmi sasa timu hiyo ya Msimbazi imetangazwa bingwa wa VPL kwa mwaka 2020/2021, huku ikiwa ni mara ya nne mfululizo.

Mechi ya mwisho ya kiporo kati ya Simba dhidi ya Coastal Union ilimalizika kwa wana wa Telanga kuibuka na ushindi wa 2-0 huku wafungaji wa magoli hayo wakiwa ni Chris Mugalu na John Bocco.

Kufuatia ushindi wa leo, John Bocco anakuwa mfungaji anaeongoza kwa magoli akiwa na 15 na kumshusha chini Prince Dube ambaye ana magoli 14 akifuatiwa na Chris Mugalu mwenye magoli 13.

Kitu kilichovutia zaidi katika mechi hii ni Offsides nyingi sana za Simba ambazo kwa marejeo ya picha nyingi kati ya hizi hazikuwa sahihi. Mwamuzi wa pembeni alionekana kufanya makosa hayo kutokana na Coastal Union kukabia juu sana.
sIMBA +cOASTAL UNION
Wachezaji wa Simba wakimzonga mwamuzi

Vijana wa Mgunda wapo nafasi ya pili kutoka mwisho wakiwa na alama 34 huku wakisaliwa na michezo miwili mkononi ambayo watalazimika kushinda zote ili kujinasua kwenye mtego wa kushuka daraja msimu huu.


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe