Baada ya tambwe kibao sana kutoka kwa msemaji wa Ruvu, Simba Sc ilihitaji dakika 90 kumthibitishia kuwa sasa ni “next level”, nafasi zilitengenezwa kwa wakati ila mwisho ubao wa matokeo ulisomeka Ruvu 0 – Simba 3.

Katika mchezo uliokuwa na vuta ni kivute, huku kabumbu safi lilisakatwa uwanjani Simba ilihitaji miguu ya dhahabu ya Nahodha John Bocco, Benard Morison na Chris Mugalu kuleta mambo makubwa!

Katika kipindi cha kwanza Simba walicheza kwa tahadhari na kujipatia goli dakika za 20’s kwa Bocco kumalizia krosi ya Miquesone, na wakalazimika kuendelea kushambulia kwa kushtukiza, huku Ruvu wakishambulia na kucheza mpira mzuri pia.

Kuingia kwa Benard Morrison kipindi cha pili akichukua nafasi ya Hassan Dilunga kulitengeneza hali ya kigugumizi kwa mabeki wa Ruvu wakajikuta wakicheza rafu za ovyo ovyo huku wakimuacha Morrison ang’ae, akitoa asisti kwa Mugalu na kusababisha Penati iliyofungwa na Bocco.

Kilichoteka hisia za watu wengi katika mchezo huu pia, ni kadi nyekundu zilizotoka. Juma Nyosso anapewa kadi kwa kumpiga kiwiko Kapombe akiwa bila mpira, Kipa anapewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Morison akiwa hana mpira.

Kwa matokeo haya Simba sasa itakuwa na alama 67, huku ikiendelea kuongoza msimamo ikiwa bado ina michezo miwili mkononi. Kasi ya kuwania kiatu cha ufungaji bora kinapamba moto, Dube – 14, Bocco – 13, Kagere – 11 na Mugalu – 10. Nani atachukua kiatu hicho, ni suala la muda tu!

MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa