Wadhamini wakuu wa ligi kuu Tanzania bara, Vodacom wameamua kujitoa kwenye udhamini wa ligi hiyo kutokana na kinachosemakana kuwa wanapata hasara kubwa kwenye udhamini huo.

Taarifa hiyo imekuja baada ya Kampuni ya Vodacom kuandika barua kwa TFF ya kueleza nia ya kuvunja mkataba wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania bara kutokana na kampuni hiyo kuyumba kimapato.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi ni kwamba Vodacom walipata hasara ya Tsh bilioni 30 kwa mwaka uliopita hivyo pamoja na mapenzi waliyonayo kwa ligi kuu ambayo imekua ikiitwa kwa jina lao, wameamua kuchukua uamuzi huo mgumu ili kubana matumizi.

Vodacom wana mkataba wa udhamini na TFF hadi msimu ujao na wamekua wakitoa zaidi ya Tsh bilioni 3 kwa mwaka.

Itakumbukwa hivi karibuni tu Azam Media Group ilisaini mkataba wa kurusha matangazo ya ligi hiyo mubashara huku ikitoa mkwanja mrefu wa bilioni 225, huku mdhamini mkuu akiwa anatoa angalia bilion 3 tofauti na zile 22.5 bn za Azam.

Je, ni wakati sahihi kwa Azam Media kupewa udhamini huo wa moja kwa moja au tusubiri subiri kwanza?


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa