Yanga Matatani Kufungiwa Miaka 3.

Zimwi likujualo, halikuli likakwisha. Ndicho kinachokwenda kuwatokea Dar es Salaam Young Africans – Yanga SC.

Baada ya kutemana na Hamis Tambwe, 2018/19. Klabu hiyo ilishtakiwa kwa kutomlipa Tambwe Stahiki zake kama ambavyo alistahili. Kwa mujibu wa kesi hiyo ambayo ilielekezwa Fifa, Yanga walipaswa kumlipa mchezaji huyo takribani milioni 43.5.

Fifa iliielekeza klabu hiyo kumlipa Tambwe na klabu ilikata rufaa ya maelekezo hayo na kupeleka sakata hilo kwenye mahakama ya kimichezo – CAS, nchini Uswisi.

CAS nayo ilitoa tamko la kuitaka klabu hiyo kumlipa Tambwe kama ambavyo Fifa ilielekeza hapo awali.

Yanga
Hamis Tambwe alipokuwa Yanga.

Tambwe alirudisha suala hilo Fifa akiomba msaada zaidi na kwa mujibu wa wakala wake – Felix Majani, Yanga wamefungiwa kufanya usajili wowote kwa kipindi cha miaka 3 mpaka pale watakapo mlipa Tambwe stahiki zake. Endapo klabu hiyo itashindwa kufanya hivyo, watakatwa pointi kwenye VPL na pia watapigwa faini kubwa zaidi.

Afisa habari wa klabu hiyo, Antonio Nugaz amethibitisha kupokea taarifa hiyo kwa kusema kuwa ” kwanza niwaondoe hofu mashabiki wa Yanga kuhusu ishu ya Tambwe, tumepokea taarifa hiyo kupitia kwa katibu mkuu wa klabu – Hajji Mfikirwa na ataifanyia kazi.

“Kama mchezaji anatakiwa kulipwa basi atalipwa bila matatizo yeyote kupitia kwa wadhamini wetu SportsPesa na Brand GSM.” aliiambia Viwanjani Leo.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA KASINO YA MERIDIANBET

Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.

Neptune's-Riches_Casino-Post_30-January

Cheza hapa

17 Komentara

    Yanga Wana wakati mgumu Sana wa kutoa pesa nyingi Sana

    Jibu

    Duhh mmeanza figisu figisu

    Jibu

    Sasa itakuwaje polen sana yanga

    Jibu

    Mlipen hak yake

    Jibu

    Pesa nyingi sana lkn inabidi wamlipe haki yake

    Jibu

    Pole yao yanga chamuhimu wampe haki yake

    Jibu

    Nomaa

    Jibu

    Yanga mnafeli wapi ??mlipeni tu hiyo ni Haki yake

    Jibu

    Wamlipe pesa zake

    Jibu

    Noma

    Jibu

    Yanga ni lazima wamlipe huyo mchezaji la sivyo itakula kwao

    Jibu

    Duuh sio poa

    Jibu

    Duh mbona hatari

    Jibu

    Hatari

    Jibu

    Kazi ipo

    Jibu

    Sa haiwezekan hela ndog kwa gsm

    Jibu

    Tena wafungiwe miaka hata sita

    Jibu

Acha ujumbe