Wanaowindwa na Man City

Kyle Walker anayecheza nafasi ya ulinzi wa klabu ya soka ya Manchester City mwenye umri wa miaka 28 anataka kurejea kwenye nafasi yake ya beki na Uingereza mara baada ya kukipiga kama kiungo cha kati na nyuma wakati wa mitanange ya kuwania Kombe la Dunia mwaka huu nchini Urusi.

Wakati huo huo, klabu yake ya Manchester City itaungana na wapinzani wao wa jadi, Manchester United kwenye mbio za kumnasa mchezaji kiungo wa kati, Frenkie de Jong kutokea Uholanzi ambapo pia wanamuwinda tena kiungo wa kati wa Paris St-Germain, Adrien Rabiot.

Rabiot alikuwa na wakati muda sana pale Etihad akiwa kama kijana na kwa sasa ni mchezaji ambaye kwa msimu ujao anatarajiwa kuendelea kukipiga kwa klabu hiyo ya Ufaransa iliyopo nafasi ya kwanza ikiwa na alama 18 kwenye Ligue 1.

Acha ujumbe