Washika Mitutu wa klabu ya Arsenal wanasemekana kuwa wanazungumza na Lorient juu ya kumsaini Matteo Guendouzi ambaye ana umri wa miaka 19 kutokea huko Ufaransa na kwa sasa yupo kwenye kikosi cha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 kwa mujibu wa Sky Sports.
Kwa upande mwingine mchezaji kiungo wa kati wa huko Uruguay mwenye umri wa miaka 22, Lucas Torreira anayetarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa afya kule Arsenal leo hii anafunguka na kusema kwamba endapo hili likifanikiwa basi yeye anahitaji kupata fursa kubwa klabuni hapo.
Bild kupitia Talksport wanasema kuwa baba wa Mesut Ozil amemwambia kiungo huyo wa kati wa Arsenal amalize taaluma yake na taifa la Ujerumani mara baada ya mchezaji huyo kulaumiwa kufuatia matokeo mabaya katika michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi.
Furahav
Habari njema.