Kocha mkuu wa Ghana Otto Addo ameamua kujiuzulu wadhifa wake hapo jana baada ya timu yake hiyo kushindwa kwenda hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Dunia kwa kupoteza kwa mabao 2-0.

 

Addo Ajiuzulu Kama Kocha Mkuu wa Ghana

Uamuzi huo umefanywa huku Otto Addo akiendelea kuwa kocha msaidizi katika klabu ya Borussia Dortmund inayoshiriki Ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga.

Ghana jana walikuwa wakihitaji matokeo kwenye mechi hiyo ili waweze kuendelea na michuano hii nchini Qatar baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya Ureno.

Mechi ya pili ya Addo licha ya kushinda jana walihitaji pia sare au ushindi lakini mpaka dakika ya 45 za kwanza kumalizika walikuwa wameshafungwa kwa mabao mawili, huku wakiwa wamekosa penati waliyopata.

Addo Ajiuzulu Kama Kocha Mkuu wa Ghana

Ilikuwa mechi ya kisasi kati yao wakikumbuka kilichotokea 2010 walipotolewa dhidi ya Uruguay katika hatua ya robo fainali, lakini jana baada ya mchezo kumalizika hakuna kati yao anayeendelea baada ya Korea Kusini kushinda.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa