Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina na vilabu vya Atletico Madrid, Manchester City, pamoja na Barcelona Sergio Aguero anaamini nyota mwezake wa timu hiyo Lionel Messi anaamini ana uwezo wa kubeba kombe la dunia.

Mshambuliaji huyo anaamini Messi ni kama alikombolewa mara tu baada ya kubeba kombe la Copa America mapema mwaka jana. Baada ya kubeba kombe hilo ilimfanya staa huyo kuanza kua na moyo wa kuipambania tena timu hiyo.agueroMessi amekua akipewa lawama kwa muda mrefu baada ya kushindwa kuipatia taji lolote timu yake ya taifa lakini baada ya kubeba taji la Copa America ilimpa nguvu tena ya kuipambania timu ya taifa ya Argentina.

Lionel Messi ambaye tayari amefunga magoli matatu kwenye michuano hii huku jana akifanikiwa kufikisha magoli tisa katika michuano ya kombe la dunia huku akimuacha gwiji wa zamani wa timu hiyo Diego Armando Maradona. Hiyo ni baada ya kufunga katika ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Australia katika mchezo wa 16 bora.

Aguero anaamini nyota mwenzake huyo ana nafasi ya kuonesha makali zaidi na kubeba taji la kombe la dunia kwani kwasasa wameshatinga hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kumfunga Australia.agueroAguero anasema Messi atapambana kwa namna yeyote kuhakikisha anabeba ubingwa wa kombe la dunia baada ya kuishi akikosolewa baada ya kupoteza fainali nne akiwa na timu hiyo, Tatu zikiwa za Copa America 2007,2016,2017 huku kombe la dunia ikiwa 2014.

Lakini kubeba taji la kombe la Copa America kulibadili taswira nzima ya Lionel Messi na akaanza kua na furaha tena ya kuipambania bendera ya nchi hiyo akiamini nyoa huyo wa zamani wa klabu ya Manchester City.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa