Kiungo wa timu ya taifa ya Morocco na klabu ya Fiorentina ya ligi kuu nchini Italia Sofyan Amrabat amesema anafurahishwa na yeye kuhusishwa na klabu kubwa barani Ulaya.
Kiungo huyo amekua kwenye rada za vilabu vingi vikubwa kwasasa kama Liverpool, Tottenham, na Atletico Madrid kutokana na ubora mkubwa aliouonesha kwenye michuano ya kombe la dunia mpaka sasa.Kiungo Sofyan Amrabat amekua nguzo muhimu kwenye kikosi cha kocha Walid Regragui wa Morocco, Kwani kiungo huyo amekua mwenye mchango mkubwa kwa timu hiyo mpaka timu hiyo inafanikiwa kufika hatua ya nusu fainali na kuweka rekodi.
Kiungo huyo amedai anafurahishwa na kuhusishwa na vilabu vikubwa lakini kwasasa yeye ni mchezaji wa klabu ya Fiorentina na anaheshimu hilo, Lakini pia ana mahusiano mazuri na rais wa klabu hiyo.Kiungo Sofyan Amrabat pia aliulizwa kuhusu kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone lakini kiungo huyo amesema wana kocha mzuri, Lakini mchezaji huyo ameeleza kua anavutiwa na aina ya ufundishaji wa kocha huyo.