Lionel Messi na  Argentina, wametinga hatua ya 16 ya Kombe la Dunia huku mchezaji huyo akisisitiza kuwa  “wameimarika” kufuatia kukosa penalti na kupata ushindi wao muhimu wa 2-0 dhidi ya Poland.

 

Argentina Yatinga Hatua ya 16 Bora Licha ya Kukosa Penati

Kikosi cha Lionel Scaloni kilijikatia tiketi ya kuingia hatua ya 16 bora, kwa kuwatungua kina Lewandowski mabao mawili kwa bila licha ya Wojciech Szczesny kuokoa penati ya Messi na baadae  mabao ya kipindi cha pili kutoka kwa Alexis Mac Allister na Julian Alvarez na kuwapeleka washindi wa Kundi C.

Argentina, ambao walipata kichapo cha kushangaza cha 2-1 kutoka kwa Saudi Arabia katika mechi yao ya ufunguzi, sasa wamefuzu kwa hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia kwa mara ya 13 katika mechi 14, na watacheza na washindi wa pili wa Kundi D Australia Jumapili.

Messi amesema kuwa; “Timu ilitoka kwa nguvu baada ya kosa langu hilo,” huku akiwa amemzidi Diego Maradona kwa kuichezea Argentina mechi nyingi zaidi za Kombe la Dunia (22).

Argentina Yatinga Hatua ya 16 Bora Licha ya Kukosa Penati

Messi amesema kuwa walifahamu kuwa goli la kwanza likiingia ndio litabadilisha mchezo, mchezo uliopita uliwapa utulivu mkubwa na wakatoka uwanjani wakifikiria kushinda, pia mchezo na Australia utakuwa mgumu sana.

Mtu yeyote atashinda kwani kila kitu ni sawa na wanapaswa kujiandaa kwa mchezo kwa njia bora wanayofanya kila wakati. Lazima wawe watulivu na kwenda na mchezo baada ya mchezo.

Argentina wanasema kuwa Kombe lingine la Dunia linaanza na wanatumai wanaweza kuendelea kudumisha kile walichonacho huku Nicolas Otamendi akikubaliana kuwa hiyo ni timu ambayo inaimarika.

Argentina Yatinga Hatua ya 16 Bora Licha ya Kukosa Penati

Huku Rodrigo De Paul akipongeza utu ulioonyeshwa na kikosi, Mac Allister anaamini uchezaji wao utaongeza imani yao kuelekea hatua ya mtoano huku akisifia kuwa ulikuwa ni mchezo mzuri wa timu.

Ilikuwa mchezo wa kuridhisha. Tunatafuta bao kila wakati. Nafikiri tulirudi kuwa timu tuliyokuwa zamani. Tuliumiliki mpira zaidi, tulikuwa na amani ya akili, na hatukukata tamaa.


Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

BONYEZA HAPA KUCHEZA

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa