Brazil Nje Kombe la Dunia

Timu ya taifa ya Brazil imetolewa rasmi kwenye michuano ya kombe la dunia na timu ya taifa ya Croatia katika mchezo wa robo fainali uliopigwa katika dimba la Education City.

Mchezo huo uliokua una kasi ulishuhudia timu hizo zikienda dakika 120 ndipo liweze kupatikana bao baada ya dakika 90 kumalizika kwa timu hizo kutokufungana kutokana na ubora mkubwa uliokua ukioneshwa na safu zote za ulinzi.brazilDakika ya 105 dakika za nyongeza alikua ni Neymar Jr ambaye aliwaeka mbele timu ya taifa ya Brazil baada ya kufunga bao zuri akipokea pasi ya Lucas Paqueta kabla ya timu ya taifa ya Croatia kusawazisha bao hilo dakika ya 117 kupitia kwa mshambuliaji wao Bruno Petrovic.

Mchezo huo uliendelea kwa kasi mpaka pale mwamuzi Michael Oliver kutoka nchini Uingereza alipoamua kumaliza mchezo huo na kuelekea kwenye mikwaju ya penati ambapo ndipo Brazil safari ilipowakuta.brazilSio mwingine ni Golikipa Dominik Livakovic aliokoa penati tatu kwenye mchezo wa 16 bora dhidi ya Japan na leo tena anafanikiwa kuokoa penati ya Rodrygo ambapo iliyowafanya wachezaji wa Brazil kuondoka mchezoni kabisa na kuwapa nguvu wachezaji wa Croatia.

Brazil walikosa penati mbili huku Croatia wakifunga penati zao nne na kuwafanya kufuzu hatua ya nusu fainali kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivo mwaka 2018 ambapo walifungwa katika mchezo wa fainali.

 

Acha ujumbe