Bruno Fernandes: Morocco Wamestahili Nusu Fainali

Kiungo wa timu ya taifa ya Ureno Bruno Fernandes amewapongeza timu ya taifa ya Morocco kwa kufuzu hatua ya nusu fainali na kusema wamestahili baada ya kuwatoa wao kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia.

Timu ya aifa ya Ureno jana ilifurushwa nje ya michuano ya kombe la dunia na timu ya taifa ya Morocco kwa kufungwa bao moja kwa bila na timu. Ambapo waliiacha timu hiyo ya taifa ya Morocco kuweka historia kua timu ya kwanza kutoka barani Afrika kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia.Bruno FernandesKatika mtandao wake wa kijamii wa Twitter Bruno Fernandes aliandika namna amejiskia vibaya baada ya kutolewa kwani kulitumikia taifa lake ni zaidi ya kucheza mpira wenyewe, Huku akieleza kua licha ya kutolewa na maumivu waliyoyapata lakini anajivunia kua Mreno na anajivunia wale wote ambao wameipambania Ureno kwenye michuano hiyo pamoja na yeye.

 

Bruno Fernandes alimalizia kwa kusema anawapongeza Morocco kwa mchezo mzuri waliouonesha na walistahili kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Al Thumama nchini Qatar.Bruno FernandesLicha ya kiungo huyo kuonesha kua muungwana na kuwapongeza timu ya taifa ya Morocco baada ya ushindi lakini kiungo huyo pamoja na mkongwe wa timu hiyo Pepe walionesha kutokuridhishwa na shirikisho kuwapangia marefa kutoka Argentina. Argentina ambapo anatoka hasimu wa nahodha wao Cristiano Ronaldo huku wao wakiona kama ni mpango maalumu wa kuwatoa kwenye michuano hiyo.

 

Acha ujumbe