David Beckham Amsifu Kane

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza David Beckham amemsifu nahodha wasasa wa timu hiyo Harry Kane na kusema ni kiongozi wa kweli.

Mchezaji Harry Kane alifanikiwa kufunga bao la kusawazisha kupitia mkwaju wa penat baada ya Bukayo Saka kuangushwa kwenye eneo la hatari huku Ufaransa wakiwa wametangulia kwa ao la mapema la kiungo Aurrelien Tchouameni.david beckhamNahodha Harry Kane alipata nafasi ya kusawazisha kupitia mkwaju wa penati tena baada ya Mason Mount kuchezewa faulo huku Ufaransa wakiongoza kwa bao la Olivier Giroud lakini mkwaju wa penati wa mshambuliaji huyo ulipaa juu ya lango.

David Beckham amempongeza Kane kwa kuonesha Uongozi kwani baada ya kupata mkwaju w kwanza wa penati ulipotokea mwingine hakusita na kuchukua mpira ule na kwenda kuupiga ila bahati mbaya hakufunga.david beckhamGwiji David Beckham aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram kua mara nyingi kuna kujiskia vibaya sana pale ambapo mnatolewa kwenye michuano, Lakini vijana wanaendelea kukua na kocha Southgate, wachezaji na mashabiki wanabidi wajivunie timu yao, Huku akisema muda mwingine watakua na mwisho wa tofauti na wanatakiwa kuinua vichw vyao juu.

Acha ujumbe