Kiungo wa Manchester City na timu ya Taifa ya Ubelgiji Kevin De Bruyne alitawazwa mchezaji bora katika ushindi wa 1-0 wa Ubelgiji dhidi ya Canada katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia hapo jana.

 

De Bruyne, De Bruyne: ” Sikucheza Mchezo Mzuri”, Meridianbet

Ubelgiji walikuwa wa pili kwa kiwango bora kwa sehemu kubwa za mchuano wa Kundi F kwenye Uwanja wa Ahmad Bin Ali, huku Thibaut Courtois akilazimika kuokoa penalti kutoka kwa Alphonso Davies kabla ya Michy Batshuayi kufunga bao lililoonekana kuwa la ushindi.

De Bruyne baada ya mchezo kuisha na kutunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo alitahamaki na kusema kuwa; “Sidhani kama nilicheza mchezo mzuri, sijui kwa nini nimepata tuzo hii labda kwa sababu ya jina langu.”

De Bruyne aliendelea kusema kuwa hawakucheza vizuri kama timu, haswa katika kipindi cha kwanza kwani walianza vibaya sana kasi ilikuwa na timu ya Canada na hawakuweza kupitia vyombo vya habari, na lukikuwa na nafasi zaidi.

De Bruyne: " Sikucheza Mchezo Mzuri"

Alisema kuwa hawakucheza mchezo mzuri akiwemo yeye, lakini walipata njia ya kushinda huku mchezaji huyo akikamilisha pasi 23 kati ya 33 na kutengeneza nafasi nne, tatu zaidi ya mchezaji yeyote.

Kocha mkuu wa Ubelgiji Roberto Martinez pia alikiri timu yake haikucheza vizuri, lakini akawasifu kwa kupata pointi tatu, na kupendekeza kuwa haikuwa bahati mbaya waliweza kushinda mchezo ambao walikuwa mbali na ubora wao.

Alipoulizwa katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mchezo kama ulikuwa mchezo mbaya zaidi kwa timu yake katika mashindano makubwa, alisema: “Inategemea kile unachopima kusema ‘mbaya zaidi je, kiufundi ulikuwa mbaya zaidi? Ndiyo. Ulikuwa mchezo mbaya zaidi? Hapana, kwa sababu ni ushindi katika Kombe la Dunia.

De Bruyne: " Sikucheza Mchezo Mzuri"

Kocha huyo alisema kuwa kushinda usipocheza vizuri hakutokei kwa bahati mbaya na ilibidi waonyeshe upande tofauti kwenye uchezaji wao na kulinda vyema na kuchanganyikiwa kwa wachezaji ni kwasababu wanajali.

Hakuishia hapo tu aliwapa heshima Canada kwa uchezaji wao waliounyesha lakini hadhani kama ilimaanisha hawakustahili kashinda. Waliwapa Canada mchezo walioutaka na kuufanya uwanja kuwa mkubwa sana lakini yote kwa yote walikuwa vizuri sana.

De Bruyne na wenzake mechi inayofuata watacheza dhidi ya Morocco siku ya Jumapili majira ya saa 10:00 jioni.

De Bruyne: " Sikucheza Mchezo Mzuri"


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

De Bruyne, De Bruyne: ” Sikucheza Mchezo Mzuri”, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa