Gwiji wa zamani wa soka nchini Brazil Ronaldo De Lima ameonesha kuwatamani baadhi ya makocha wakubwa barani ulaya kuifundisha timu ya taifa ya Brazil ambayo imekua haifanyi vizuri kwasasa.
Baada ya timu ya taifa ya Brazil kutolewa kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar na alyekua kocha wa timu hiyo Adenor Leanardo Bacchi Tite kujiuluzu, Kumeibuka taarifa mbalimbali juu ya nani anastahili kua kocha mkuu wa timu hiyo.Gwiji wa zamani wa timu hiyo Ronaldo De Lima akifanya mahojiano na kituo kimoja ameonesha nia yake ya dhati ya kuhitaji baadhi ya makocha wakubwa barani ulaya kuifundisha timu hiyo, Huku akiwataja makocha kama Pep Guardiola, Carlo Ancelotti pamoja na Jose Mourinho kutoka klabu ya As Roma.
Gwiji huyo ameonesha matamanio hayo huku akisema hajui shirikisho la soka nchini Brazil linalojulikana kama CBF lenyewe linafikiria nini juu ya kocha mpya wa Samba Boys atakaevaa viatu vya kocha Tite aliyejiuzulu punde baada ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la dunia.Brazil imetimiza miaka 20 sasa tangu wafanikiwe kutwaa taji hilo mwaka 2002 pale Korea na Japan huku gwiji huyo akiwa sehemu ya kikosi kilichotwa ubingwa, Jambo la timu hiyo kutokufanikiwa kwa muda mrefu kwenye kombe la dunia limekua likiwaumiza mashabiki wengi wa timu hiyo duniani kote.
Ronaldo De Lima yeye anaamini angekua ana mamlaka ya kuteua kocha wa timu hiyo basi angechagua moja ya makocha wakubwa ulaya ambao aliwataja, Lakini pia gwiji huyo ameweka wazi kua atatoa ushirikiano kwa kocha yeyote wa kigeni atakaeifundisha timu hiyo kwasasa endapo shirikisho litachagua kocha mgeni.