Kiungo wa kati wa Denmark Thomas Delaney ameondolewa kwenye mechi zilizosalia za Kombe la Dunia baada ya kulazimishwa kutolewa nje na jeraha katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi D dhidi ya Tunisia.

 

Delaney Kutoshiriki Michuano Yote ya Kombe la Dunia

Mchezaji huyo wa Sevilla alianza kwa timu ya Kasper Hjulmand katika mchezo wa sare ya bila kufungana siku ya Jumanne katika Al Rayyan lakini akatoka kwenye mchezo baada ya kuapata majeraha kipindi cha kwanza na nafasi yake ikachukuliwa na Mikkel Damsgaard.

Ilithibitishwa siku ya Jumatano kwamba Delaney mwenye umri wa miaka 31 amepata jeraha la goti ambalo sio tu kwamba linapunguza ushiriki wake mara moja lakini linaelezea mwisho wa mchuano wake, huku ikiwa ni pigo kwa Denmark.

Hjulmand alisema kuwa; “Tutamkosa, ndani na nje ya uwanja, wachezaji wengine wako tayari na tuna kikosi imara kwaajili ya mechi zinazofuata.”

Delaney Kutoshiriki Michuano Yote ya Kombe la Dunia

Mkongwe huyo  mwenye mataji 72, Delaney alikuwa mtu muhimu katika mbio za Taifa hadi nusu fainali ya Euro 2020 kufuatia mshtuko wa moyo wa Christian Eriksen mwaka jana, huku mchezaji huyo wa Manchester United akiwa amepona na kurejea uwanjani, na timu ya Denmark ikitajwa kuwa mshindani wa taji hilo kabla ya michuano.

Delaney na timu yake ya Denmark wameanza michuano ya Kombe la Dunia kwa kutoshana nguvu na Tunisia katika kundi D, huku mechi yao inayofuata watamenyana dhidi ya Watetezi Ufaransa Novemba 26, kabla ya kukutana na Australia siku nne baadae.

Delaney Kutoshiriki Michuano Yote ya Kombe la Dunia


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Delaney, Delaney Kutoshiriki Michuano Yote ya Kombe la Dunia, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa