Mchezaji wa FC Barcelona Memphis Depay ameiambia Barcelona kuwa anataka kuondoka kwa miamba hao wa Uhispania kwa uhamisho huru baada ya Kombe la Dunia ambalo linalotarajiwa kupigwa Qatar.

 

Depay Anataka Kuondoka Barca Baada ya WC

Depay mwenye miaka  28, amecheza mara mbili pekee kwenye LaLiga msimu huu, akionekana kutokuwa chaguo la kocha wa Barcelona Xavi Hernandez huku pia akisumbuliwa na tatizo la paja.

Licha ya kukosa muda wa kucheza, mshambuliaji huyo anaelekea Qatar akiwa kama mshambuliaji tegemezi wa katika kikosi cha Louis van Gaal cha Uholanzi na The Express inaripoti kwamba hana furaha na hali yake ya Catalunya.

Taarifa kutoka Uhispania zinasema kwamba  Depay  ambaye alikuwa mfungaji bora wa pamoja katika kufuzu kwa Kombe la Dunia la Uropa na mabao 12  hivi karibuni anaweza kupangwa kurejea Ligi ya Uingereza huku Manchester United, Chelsea na Tottenham zikivutiwa nae.

Depay Anataka Kuondoka Barca Baada ya WC

Hata hivyo, aliendelea kufurahia muda mwingi akiwa na Ligue 1 Lyon baada ya kuondoka United na Erik ten Hag ana nia ya wazi ya kumpa raia wake nafasi ya pili ya kung’ara huko Manchester.

Kwa Chelsea, kufumania nyavu imekuwa ngumu msimu huu huku Raheem Sterling akiongoza orodha ya wafungaji bora wa Ligi kuu ya Uingereza akiwa amefunga mabao matano.

Depay angetoa kina zaidi katika safu ya washambuliaji ya Graham Potter na ameonekana kuwa na kiwango cha juu zaidi, akijivunia mabao 42 katika mechi 81 za Kimataifa akiwa na Uholanzi.

Depay Anataka Kuondoka Barca Baada ya WC

Iwapo akiendelea kung’ara kwenye Kombe la Dunia, hata hivyo, inaonekana kuna uwezekano kwamba Barca hawatadai ada kutoka kwa wawaniaji watarajiwa.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa