Deschamps: Tulikua na Bahati dhidi ya Uingereza

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amesema kuna vitu vidogo na bahati ndio iliwasaidia kupata ushindi dhidi ya timu ya taifa ya Uingereza katika mchezo wa robo fainali ya kombe la dunia.

Timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali baada ya kuitupa nje timu ya taifa ya Uingereza baada ya kuifunga mabao mawili kwa moja katika mchezo huo wa robo fainali uliopigwa katika dimba la Al Bayt.deschampsMabao ya Aurellien Tchouameni na Olivier Giroud yalitosha kuifikisha Ufaransa katika nusu fainali ya kombe la dunia mwaka 2022 huku bao la mshambuliaji Harry Kane kupitia mkwaju wa penati likiwa bao pekee kwa timu ya taifa ya Uingereza.

Licha ya kocha Deschamps kuamini kuamini timu yake ilikua na ubora mkubwa lakini alisisitiza kua wapinzani wao walikua wana timu nzuri na imara pia japokua wao maelezo madogo na bahati ilikua upande wao ndio maana wamefanikiwa kufuzu katika hatua ya nusu fainalideschampsKikosi cha timu ya timu ya taifa ya ufaransa chini ya mwalimu Didier Deschamps kitakwenda kucheza mchezo wa nusu fainali katika michuano ya kombe la dunia dhidi ya Morocco ambayo imewatupa nje timu ya taifa ya Ureno.

Acha ujumbe