Kocha mkuu wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps amewaomba Wafaransa waelewe zaidi kuwa timu hiyo inasonga mbele licha ya kukabiliwa na majeraha kwa baadhi ya wachezaji na kulenga malengo yao waliyojiwekea hapo awali.
Ufaransa walikuwa tayari bila Paul Pogba na N’Golo Kante kwa Kombe la Dunia na sasa wamewapoteza Christopher Nkunku na Karim Benzema usiku wa kuamkia mchuano huo.
Mabingwa watetezi wa kombe la Dunia LA 2018 wanaelekea katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Australia huku kukiwa na sintofahamu kuhusu kikosi chao, ingawa Deschamps hana wasiwasi hata kidogo kuhusu utimamu wa Eduardo Camavinga na alithibitisha Raphael Varane yuko sawa kuanza.
Alipoulizwa siku ya Jumatatu ikiwa Ufaransa italazimika kufikiria upya mbinu zao kuelekea fainali hizo, Deschamps alikataa, ingawa aliviomba vyombo vya habari vilivyokusanyika kumuunga mkono.
Kocha huyo alisema kuwa; “Ni furaha kubwa mbele na timu tuliyo nayo, tunajua Australia vizuri sana, lakini licha ya matatizo yetu Ufaransa haina wasiwasi hata huku washindi watatu wa Kombe la Dunia wakitoka katika raundi ya kwanza.
Kilicho muhimu ni kuzingatia mchezo wa kwanza dhidi ya Australia ambapo kila kitu kipo sawa na wanaangazia kushinda mchezo huo ambao uliopo mbele yao. Mchezo huo utapigwa majira ya saa nne usiku.
Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.
BONYEZA HAPA