Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amezungumza na kusema hawatacheza ili staa wa Argentina asibebe kombe la dunia katika mchezo wa fainali ya kombe hilo hapo kesho.

Lionel Messi ambaye amekua kwenye kiwango bora sana tangu michuano ya kombe la dunia lianze akiwa amehusika kwenye magoli nane mpaka sasa, Tayari akiwa amefunga mabao matano na kupiga pasi tatu za mabao.

Nahodha huyo wa Argentina anahitaji kushinda mchezo wa fainali dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa hapo kesho ili kutengeneza rekodi zaidi kwani ndo kombe pekee ambalo hajawahi kubeba, Pia kupigia msumari mjadala wa kua mchezaji bora wa muda wote.

Kocha Deschamps anasema wao hawana wasiwasi wowowte kuelekea mchezo wa fainali, Zaidi anaamini wamefanya kazi kubwa mpaka kufika hapo walipo na watafanya kila liwezekanalo kushinda mchezo wa fainali.

Didier Deschamps anajua kua watu wengi duniani na hata baadhi ya wafaransa wanatamani kuona Messi anabeba kombe la dunia, Lakini kocha huyo ameweka wazi kua hilo sio changamoto kwao zaidi watacheza kucheza kushinda mchezo huo na sio kucheza kwasababu ya kuhakikisha Messi hashindi taji hilo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa