Kiungo wa kati wa Manchester United Bruno Fernandes amesisitiza kuwa mpira wa miguu ni wa kila mtu huku mechi akijiandaa kucheza Kombe la Dunia lijalo nchini Qatar akiwa na timu yake ya Taifa ya Ureno.

 

Fernandes: 'Soka Ni la Kila Mtu'

Ligi kadhaa kubwa Duniani zitachukua mapumziko katikati ya msimu kwa ajili ya michuano hiyo inayochezwa Novemba na Desemba badala ya ile iliyozoeleka ya Juni na Julai kutokana na hali ya hewa nchini Qatar.

Pamoja na kupangwa kwa muda, kumekuwepo na mashaka kadha wa kadha kuhusu uamuzi wa kuiruhusu Qatar kuandaa michuano hiyo mikubwa zaidi ya soka, ikiwa ni pamoja na masuala ya haki za binadamu nchini humo, ikiwamo taarifa za vifo vya wafanyakazi wahamiaji wakati wa ujenzi wa viwanja hivyo.

Michuano hiyo itaanza Novemba 20, na akizungumza baada ya United kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Fulham katika mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu kabla ya hapo, Fernandes hakusita kutoa maoni yake alipozungumza na Sky Sports.

Fernandes: 'Soka Ni la Kila Mtu'

“Bila shaka ni ajabu sio wakati hasa tunataka kucheza Kombe la Dunia. Ni wazi nadhani kwa kila mtu, wachezaji, mashabiki, sio wakati mzuri zaidi kwa sababu watoto watakuwa shuleni, watu watafanya kazi, wakati hautakuwa bora kwa watu kutazama michezo.”

Fernandez hajafurahishwa na tukio la watu kufariki wakati wa maandalizi ya Kombe hilo, anasema kuwa wanataka soka liwe la kila mtu, kila mtu ajumuishwe na ashirikishwe kwenye Kombe la Dunia kwasababu ni “Dunia”, ni ya kila mtu.

Vijana wa Erik ten Hag walipata ushindi wa dakika za lala salama katika uwanja wa  Craven Cottage hapo jana kupitia kwa mchezaji wao Alejandro Garnacho, baada ya Christian Eriksen kuwapa Mashetani Wekundu uongozi wa kipindi cha kwanza kwa bao lake la kwanza kwa klabu.

Fernandes: 'Soka Ni la Kila Mtu'

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Denmark pia atakwenda Qatar, na akasema: “Ni soka, haijalishi ni wapi. Ndiyo maana tulikuwa tunaenda Kombe la Dunia, kwa sababu tulifuzu na tutacheza soka tu.”


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa