Mchezaji wa Manchester City Phil Foden amesema kuwa bado Uingereza haijaona kiwango chake bora, hivyo ameapa kuonyesha kiwango hicho kwenye michuano hii na kueleza kuwa nia yake ya kufikia viwango vya Neymar na Kylian Mbappe.

 

Foden Ameapa Kuonyesha Kiwango Bora Kombe La Dunia

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anaelekea kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar baada ya kampeni nzuri hadi sasa akiwa na Manchester City, akifunga mabao saba na kutoa asisti tatu katika mechi 14 katika michuano yote.

Foden anatazamia kuhamishia kiwango chake ambacho anacho City hadi kwenye kiwango cha Kimataifa, ambapo anahisi bado hajacheza katika kiwango chake cha juu zaidi, na amekanusha mapendekezo yake kuwa analinganishwa na Messi na Neymar ingawa anatamani kuwa kama wao katika siku zijazo.

Foden alisema kuwa; “Watu ambao umewataja hapa wako juu zaidi yangu kwa sasa, lakini napenda kufikiria kuwa naweza kuwa huko siku moja. Yote ni kuchukua hatua ndogo katika mwelekeo sahihi, nataka tu kuchukua fomu yangu ya klabu kwenye timu ya Taifa. Kwa kiwango cha klabu yangu mwaka huu, nimekuwa nikifunga mabao mengi na nataka kuleta ubora wangu”

Foden Ameapa Kuonyesha Kiwango Bora Kombe La Dunia

Mchezaji huyo aliendelea kusema kuwa lazima afunge katika michezo mikubwa na fainali kubwa ili awe na kiwango cha Dunia, aliongeza kwa kusema kuwa anajua ana uwezo wa kufanya hivyo, kwahiyo ni kitu anachojitahidi na kukitarajia.

Pia Phil hadhani kama ni rahisi kuingia katika timu na kutowajua wachezaji vizuri. Lazima ajifunze kucheza na wachezaji tofauti na kile wanachokipenda zaidi, amekuwa na uzoefu wa kutosha katika timu ya Uingereza kuwaelewa wachezaji, na ana tumai anaweza kuleta hilo kwenye Kombe la Dunia.

Foden Ameapa Kuonyesha Kiwango Bora Kombe La Dunia

Foden anasema kuwa alipaswa kufunga mabao mengi zaidi kwa Uingereza, kwani wana ubora katika kila eneo la uwanja kwahiyo hawawezi kumtegemea Harry Kane kila wakati kila wakati kwasababu timu zitajaribu kumchunga kwasababu ya ubora wake.

Uingereza wataanza kampeni yao ya Kombe la Dunia Jumatatu dhidi ya Iran, kisha kumenyana na Marekani na Wales katika Kundi B.

 

Foden Ameapa Kuonyesha Kiwango Bora Kombe La Dunia

 

Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Foden, Foden Ameapa Kuonyesha Kiwango Bora Kombe La Dunia, Meridianbet

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa