Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa anayekipiga katika klabu ya Ac Milan ya nchini Italia Olivier Giroud amefanikiwa kuweka rekodi ya kua mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Ufaransa baada ya kufikisha mabao 52.

Olivier Giroud ambaye alikua na mabao 50 mpaka michuano ya kombe la dunia inaanza akiwa nyuma ya gwiji Thiery Henry ambaye alikua na mabao 51, Lakini mshambuliaji huyo alivunja rekodi hiyo bada ya kufunga bao moja katika mchezo wa kwanza dhidi ya Australia na kumfikia Henry.giroudNyota huyo mwenye umri wa miaka 36 na siku 53 anakua mchezaji wa pili mkubwa kufunga mabao mawili katika michuano ya kombe la dunia baada ya gwiji wa soka kutoka nchini Cameroon kufanya hivyo mwaka 1998 akiwa na umri wa miaka 38.

Staa huyo ameweka rekodi yake leo baada ya kufunga goli la uongozi katika mchezo wa 16 bora dhidi ya Poland na kufanikiwa kufikisha mabao 52 hivo kuivuka rekodi ya Henry ya mabao 51 na kua mfungaji bora wa muda wote a nchi hiyo mpaka sasa.giroudGiroud ambaye alionekana hatakua na nafasi kwenye kikosi hicho baada ya Karim Benzema na Christopher kuwepo kwenye kikosi hicho, Lakini nyota huyo amekua msaada kwa timu hiyo baada ya nyota hao kuondolewa kikosini baada ya kukubwa na majeraha.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa