Lahm: Ujerumani ijipange upya

Gwiji wa zamani soka nchini Ujeruman na mshindi wa kombe la dunia na timu ya taifa ya Ujerumani Philip Lahm amesema timu hiyo inabidi kujipanga upya baada ya kutolewa kwenye hatua ya makundi kwenye kombe la dunia.

Ujerumani ambayo ilitupwa nje kwenye michuano ya kombe la dunia baada kumaliza na alama nne sawa na Hispania ambayo ilikua inaongoza kwenye magoli ya kufunga na kufungwa. Licha kupata ushindi wa mabao manne kwa mawili ili haikutosha kuwapitisha Ujerumani kwenda hatua ya mtoano.lahmHii inakua ni mara ya pili mfululizo kwa timu ya taifa ya Ujerumani kutolewa kwenye hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Urusi 2018 na mwaka huu hali imejirudia tena nchini Qatar.

Gwiji Lahm anaamini Ujerumani imekosa mipango thabiti kwenye michuano hiyo na kusababisha kutolewa japo walikua na timu nzuri, Gwiji huyo anaamini timu Ujerumani inashindwa kucheza mchezo unaomkosesha pumzi mpinzani ndio sababu ya wao kufungwa mabao.lahmLahm aliitolea mfano Argentina ambayo ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Saudia Arabia lakini ilirudia kwa nguvu na kushinda michezo yake yote miwili iliyobakia na kufuzu. Kitu ambacho anaamini Ujerumani walikikosa kwani baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Japan walikua wana uwezo wa kurudi na kushinda michezo iliyobakia na kufuzu.

Gwiji huyo anaamini kuna namna timu yao ilikosa mipango thabiti na upambanaji wa kiwango cha juu jambo lililowafanya kutolewa kwenye michuano na kuwataka kujipanga upya tena vizuri.

Acha ujumbe