Golikipa wa Tottenham Hot Spurs Hugo Lloris anaamini kwamba wachezaji lazima wazingatie soka kwenye Kombe la Dunia ambapo yeye akiwa ni moja ya magolikipa waliochaguliwa kuichezea Ufaransa.

 

 Lloris Anataka Kujikita na Kombe la Dunia Zaidi

Qatar imeangaziwa muda mrefu kabla ya mchezo wa kwanza wa michuano hiyo siku ya Jumapil, huku Lloris kiwa ni moja ya makipa wataovaa kitambaa cha unahodha kuelekea Kombe la Dunia kuiwakilisha Ufaransa.

Hata hivyo, nahodha huyo wa Les Bleus anakubaliana na maoni ya FIFA kwamba wachezaji wanapaswa kuheshimu imani ya nchi mwenyeji huku akiwasihi wachezaji kuangazia zaidi soka.

“Tunapokaribisha wageni Ufaransa tunataka wafuate sheria zetu na kuheshimu utamaduni wetu, nitafanya vivyo hivyo nikienda Qatar, tunaweza tusikubaliane na hilo, lakini nitaonyesha heshima.”

 Lloris Anataka Kujikita na Kombe la Dunia Zaidi

Lloris anaenda kushiriki Kombe la Dunia huku timu yake ya Kifaransa ikiwa ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo ambalo walilichukua mwaka 2018 baada ya kumtungua Crotia na wachezaji wake kujizolea umaarufu mkubwa huko Urusi akiwemo Kylian Mbappe.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa