Kocha mkuu wa Uhispania Luis Enrique anaamini kuwa Gavi atakuwa mmoja wa “mastaa wa soka” baada ya kijana huyo kufunga bao lake la kwanza la Kombe la Dunia Uhispania ilipoichabanga Costa Rica mabao  7-0 hapo jana.

 

Luis Enrique: "Gavi Atakuwa Nyota wa Mpira"

Gavi alifunga bao la tano katika pambano lao la jana, akimalizia pasi ya Alvaro Morata huku zikiwa zimesalia dakika 16 kumalizika kwa mpira.

Gavi ambaye ana umri wa miaka 18 na siku 110, imemfanya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao kwenye Kombe la Dunia kwa Taifa hilo tangu Pele alivofanya hivyo akiwa na miaka 17 na siku 249 akiwa na Brazil katika fainali ya 1958 dhidi ya Uswidi.

Luis Enrique: "Gavi Atakuwa Nyota wa Mpira"

Baada ya ushindi wa mabao hayo 7-0  katika kundi E kocha Luis aliulizwa na waandishi wa habari jinsi kiungo huyo wa Barcelona anavyoweza kuwa mzuri zaidi alisema; “Sijui, natumai anaenda na kucheza kila wakati vizuri zaidi na kujaribu kuwa bora zaidi na bila mpira yeye ni wa kipekee, na tofauti sana kwasababu ana miaka 18 sasa, lakini ana tabia ya kuwa mchezaji mwenye uzoefu.”

Luis aliendelea kwa kusema uwa ni furaha kuwa na mchezaji kama huyo kwasababu bado ni mdogo, anahitaji utulivu kidogo wakati mwingimne lakini wanafuraha sana kuwa naye katika timu na anadhani kuwa atakuwa mmoja wa nyota wa soka.

Luis Enrique: "Gavi Atakuwa Nyota wa Mpira"

Mechi inayofuata ya Luis watakipiga siku ya Jumapili nchini Qatar dhidi ya Ujerumani, ambayo imetoka kuchapwa kwa mabao 2-1 na Japan mapema hapo jana majira ya saa 10:00 licha ya kutangulia kwa bao moja.


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Luis, Luis Enrique: “Gavi Atakuwa Nyota wa Mpira”, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa