Luis Suarez ametuma pongezi zake kwa mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona Lionel Messi baada ya nyota huyo wa Argentina kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Dunia.
Messi alifunga bao moja kwa mkwaju wa penati na kutoa pasi nzuri iliyotengeneza bao la pili la Julian Alvarez katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Croatia, na hivyo kuwaweka Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia ambapo watakutana na Ufaransa au Morocco.
Bashiri na kitochi au bila bando mechi hii, Bonyeza hapa kutazama ODDS kubwa na bomba kupitia machaguo spesho ya meridianbet ili kuingia mchezoni. Pia ukibashiri na kitochi kwa dau la TZS 1,000/= Unaweza kuibuka mshindi wa MBUZI WA KITOWEO CHA SIKUKUU, kila wiki Ijumaa.
Asisti yake ndiyo iliyonyanyua mchezo wakati akikimbia kutoka karibu na mstari wa katikati hadi kwenye sanduku la penati, na kumpa Josko Gvardiol – bila shaka beki chipukizi bora zaidi duniani wakati mgumu, kabla ya kumtengenezea Alvarez wa Manchester City kufunga.
Baada ya mchezo huo, wachezaji wakubwa wa soka duniani walimmiminia sifa Messi, ambaye ni ushindi mmoja tu baada ya kutwaa tuzo pekee ambayo imemponyoka katika maisha yake ya kihistoria na anayoitaka zaidi, ya Kombe la Dunia.
Rafiki yake wa zamani Suarez, ambaye alishiriki naye maisha akiwa Barcelona na kuendeleza uhusiano wa karibu naye ndani na nje ya uwanja, alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kumpongeza supastaa huyo wa Argentina.
“Huchoki kuonyesha kuwa wewe ndiye bora zaidi ulimwenguni,” mshambuliaji huyo wa Uruguay alisema kwenye Instagram baada ya mchezo.
“Kwamba kila mtu asimame kupongeza kile kijana huyu [Messi] anatoa kwa mpira wa miguu. Inavutia rafiki yangu.”
Wawili hao walikuwa Barcelona kwa miaka sita kati ya 2014 na 2020 na walishinda mataji kadhaa pamoja, ikiwa ni pamoja na treble ya ligi, kombe la Ligi ya Mabingwa mwaka 2015, na kuunda muunganiko maarufu na Neymar, iliyoitwa ‘MSN’, ambayo ilikuwa yenye nguvu zaidi, utatu bora katika soka.
Messi alikuwa akimtetea Suarez wakati Muruaguay huyo alipoondoka Barcelona kwa utata, akihisi hakuheshimiwa alipokuwa akitoka, na hicho kilikuwa kipimo cha uhusiano wao.
Wawili hao pia ni marafiki nje ya uwanja, mara nyingi hushiriki picha za likizo pamoja na wapenzi wao na kuzunguka miji mbalimbali.