Klabu ya Real Madrid ambayo ipo chini ya kocha mkuu Carlo Ancelotti wanahitaji kuongeza mshambuliaji katika kikosi chao kufuatia jeraha alilopata mchezaji wao nambari 9 Karim Benzema akiwa kwenye majukumu ya Kimataifa nchini Qatar.

 

Madrid Waanza Mbio za Kumsaka Raphael Leao Januari

Benzema ambaye ana miaka 34, alipata jeraha la paja akiwa mazoezini kabla ya mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa dhidi ya Australia hapo kesho. Mshindi huyo wa Ballon d’Or tayari amekosa mechi tisa hadi sasa na bado ndiye mshambuliaji pekee anayetambulika kwa Ancelotti.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uhispania, Ancelotti amemshawishi rais wa klabu hiyo Florentino Perez kwamba mabingwa hao wa Ulaya wanahitaji kutafuta mbadala wa Benzema ili waweze kutetea taji lao msimu huu.

Madrid Waanza Mbio za Kumsaka Raphael Leao Januari

Real Madrid wapo pointi mbili nyuma ya Barcelona kwenye LaLiga, wakati watamenyana na Liverpool katika mechi ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa mwezi Februari, huku mchezaji wa AC Milan Raphael Leao 23, akiwa ni chaguo la kocha huyo.

Leao anatazamiwa kuanza kampeni yake ya Kombe la Dunia wakati washindi wa Euro 2016 watakapomenyana na Ghana siku ya Alhamisi. Lakini pia mshambuliaji wa Argentina na Inter Milan Lautaro Martinez, 25 anawindwa pia.

Madrid Waanza Mbio za Kumsaka Raphael Leao Januari

Martinez amefunga mabao saba katika mechi 15 za Serie A msimu huu na amefunga mabao 21 katika mechi 40 za Kimataifa akiwa na Argentina.


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Madrid, Madrid Waanza Mbio za Kumsaka Raphael Leao Januari, Meridianbet

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa