Shirikisho la Soka la Senegal limethibitisha kuwa mchezaji wa FC Bayern Munich na timu ya Taifa ya Senegal Sadio Mane ameondolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia kutokana na jeraha la mguu alililolipata.

 

Mane Atalikosa Kombe la Dunia

Mane alikabiliwa na tatizo hilo kwenye mchezo wao wa ligi walipokuwa wakikabiliana na Werder Bremen ingawa alionekana kuwa sawa vya kutosha na kujumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 26 cha Aliou Cisse kitakachoshiriki Kombe la Dunia.

Ilitangazwa Jumanne kwamba Mane hatashiriki katika mechi za ufunguzi za Senegal, timu ya Cisse ikisema “itategemea kucheza mechi za kwanza bila Sadio.

Mane Atalikosa Kombe la Dunia

Lakini Shirikisho la Soka la Senegal hapo jana lilithibitisha kuwa jeraha la kiungo huyo litahitaji kufanyiwa upasuaji, na hivyo kumfanya kuwa nje ya michuano yote ambayo watacheza wakiwa Qatar, huku Shirika hilo likimtakia ahueni ya haraka mchezaji huyo.

Inakuja kama pigo kubwa kwa mchezaji huyo na Senegal baada ya kushiriki pamoja katika ushindi wao wa Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) kwa kufunga mikwaju ya penalti ya ushindi katika fainali dhidi ya Misri mnamo Februari.

Mane Atalikosa Kombe la Dunia

Senegal itamenyana na Uholanzi katika mechi ya kwanza ya Kundi A Jumatatu kabla ya kukutana na Qatar na Ecuador, ingawa itabidi   ijaribu kufika hatua ya mtoano bila mshambuliaji wao nyota amabye ndiye tarajio la watu wengi kumuona huko Qatar.

Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Mane, Mane Atalikosa Kombe la Dunia, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa