Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane imeelezwa ataukosa mchezo wa kwanza wa kombe la dunia wa taifa lake dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi bvaada ya kupata majeruhi siku kadhaa nyuma.

Mchezaji huyo ambaye alikua anahofiwa kukosa michuano hiyo baada ya kuumia kwenye mchezo wa ligi kuu ya Ujerumani dhidi ya klabu ya Wder Bremen kwenye ushindi wa mabao sita kwa moja ambao klabu ya Bayern Munich ilioupata.maneLicha ya kupata majeraha ambayo yalikua hatarishi kwa mchezaji huyo kukosa michuano hiyo lakini alijumuishwa kwenye likosi cha Senegal chini ya mwalimu Alliou Cisse kutokana na umuhimu wake ndani ya kikosi cha taifa hilo.

Mane ataanza kutumika katika mchezo wa pili wa kundi A dhidi ya wenyeji Qatar kabla ya kumaliza dhidi ya Ecuador tarehe 29 mchezaji huyo alikua na nafasi ya kukutana na mchezaji mwenzake wa zamani wa klabu ya Liverpool Virgil Van Dijk.mane, Mane kuwakosa Uholanzi Qatar, MeridianbetSadio Mane amekua nguzo kubwa kwenye timu ya taifa ya Senegal kutokana na uwezo mkubwa ambao amekua akiuonesha kwenye timu hiyo, Huku akifanikiwa kuisaidia timu hiyo kubeba ubingwa wa Afrika pamoja na kufuzu michuano ya kombe la dunia.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa