Beki wa kushoto wa klabu ya Real Madrid na Raia wa Ufaransa Ferlan Mendy ameachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kitakachokwenda kushiriki michuano ya kombe la dunia mwezi huu nchini Qatar.

Kukosekana kwa jina la beki huyo imezua mijadala kwa wapenzi na wadau wa soka nchini Ufaransa kutokana na kiwango ambacho amekua akionesha beki huyo ndani ya klabu ya Real Madrid.mendyKocha wa timu ya taifa ya Ufaransa amewaita ndugu wawili ambao wamekua wakicheza nafasi ya beki wa kushoto Lucas Hernandez anayecheza klabu ya Fc Bayern Munich pamoja na Theo Hernandez anayecheza katika klabu ya Ac Milan mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Italia.

Pamoja na mabeki hao kucheza kwa kiwango cha juu kwa mabeki hao kwenye vilabu vyao, lakini wengi wanaamini nafasi ya Ferlan Mendy alistahili kuwepo kwenye kikosi hicho chini ya mwalimu Deschamps.

Beki huyo amekua akionesha ubora mkubwa katika klabu ya Real Madrid na kuweza kuisaidia klabu hiyo kubeba mataji mbalimbali huku akiwa ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Real Madrid.mendyMara kadhaa Mendy amekua sio chaguo la mara kwa mara la mwalimu Deschamps kitu ambacho kimewafanya watu wengine kutokushangazwa kutokana na maamuzi yaliyofanyika jana na kocha huyo kumtema beki huyo.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa