Lionel Messi amesema kuwa maendeleo ya Argentina hadi kufika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia ni msukumo kutoka kwa Gwiji wa Taifa hilo Diego Maradona kutoka mbinguni.
Argentina haijashinda michuano hiyo tangu Maradona alipoongoza ushindi wao wa pili mwaka 1986, na hii ni fainali ya kwanza tangu aondoke miaka miwili iliyopita.
Nahodha wa Argentina Messi kwa muda mrefu amekuwa akilinganishwa na mchezaji mwingine bora wa 10 wa nchi hiyo, huku uchezaji wake nchini Qatar ukihimiza matumaini ya kutwaa taji la tatu lililokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu.
Messi alitoa pasi ya mabao kwa Nahuel Molina dhidi ya Uholanzi katika robo fainali ya hapo jana kisha akaiongezea timu yake bao la pili kwa mkwaju wa penalti, lakini Argentina walipata hofu kubwa kwani mabao mawili ya Wout Weghorst yalipelekea sare hiyo kuwa ya mikwaju ya penalti.
Emiliano Martinez aliokoa mipira miwili, na kuiruhusu Argentina kupenya kabla ya kusherehekea uwanjani mbele ya mashabiki wao huku Maradona akiwa maarufu katika mawazo yao.
Messi amesema kuwa; “Tunaacha hilo uwanjani na watu wetu, walifurahia wakati huo hapa na timu hiyo. Watu wamejawa na shauku sisi ni miongoni mwa waliofuzu kwa nusu fainali na sasa tuna uzito kutoka kwa mabega yetu na tumekuwa tukisema hivi tangu mwanzo.”
Messi alijua jinsi Argentina walivyokaribia kuondolewa, ingawa hakuhisi mechi hiyo ingeenda mbali hivyo kwani bao la pili la Weghorst lilitokana na mkwaju wa faulo uliozua utata wa dakika ya 101.
Messi aliongeza kusema kuwa hataki kuongelea waamuzi, unaweza kuadhibiwa na huwezi kuwa mkweli kwani hakuwa kwenye kiwango na alikuwa mkali kwao Lautaro Martinez alipofunga, kulikuwa na uzito mkubwa kwenye vifua vyao.