Luka Modric amesisitiza kuwa Croatia haiko kwenye Kombe la Dunia ili tu kushiriki huku akitaja kuwa wana matamanio makubwa licha ya kuanza michuano hii bila ushindi dhidi ya Morocco.

 

Modric Asisitiza Kuwa Croatia Itakuwa Bora

Modric na timu yake ambao ndio washindi wa pili wa Kombe la Dunia la 2018 baada ya kupoteza fainali mbele ya Ufaransa miaka minne iliyopita, azma yao ni kwenda hatua ya ziada nchini Qatar kwenye michuano hii.

Croatia imeshindwa kufunga bao kwenye mchezo wao wa kwanza na kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Morocco kwenye Kundi F ambalo kinara ni Ubelgiji mpaka sasa.

Lakini nahodha huyo anasisitiza kwamba kuna mengi zaidi yatatoka kwa upande wa Zlatko Dalic, ambao wamepata kipigo kimoja tu tangu walipotoka kwenye michuano ya Euro 2020 dhidi ya Uhispania mwaka jana.

Modric Asisitiza Kuwa Croatia Itakuwa Bora

Modric amesema kuwa; “wakati Kombe la Dunia likiendelea, Croatia itakuwa bora na hatukuja hapa kushiriki tu. Matarajio yetu ni makubwa, lakini tunapaswa kuyachukua hatua kwa hatua.”

Amesisitiza kuwa hataki kueleweka vibaya kufikia mzunguko wa pili sio lengo lao pekee, la kwanza tu malengo yao ni makubwa zaidi. Mchezaji huyo ameichezea Croatia mechi nyingi zaidi za michuano mikubwa kuliko mchezaji mwingine yoyote (26), na kutengeneza historia zaidi licha ya Taifa lake kuanza bila ushindi.

Akiwa na umri wa miaka 37 na siku 75, kiungo huyo wa kati wa Real Madrid alikua mchezaji mkongwe zaidi wa Taifa lake kuwahi kucheza Kombe la Dunia, vilevile akawa mchezaji wa kwanza kutokea katika michuano ya Ulaya na Kombe la Dunia katika miongo mitatu tofauti.

Modric Asisitiza Kuwa Croatia Itakuwa Bora

Modric na wenzake, ambao pia wanamenyana na Canada na Ubelgiji katika Kundi F, wametoka katika hatua ya makundi au wametinga nusu fainali katika mechi zao tano za awali kwenye fainali hizo.


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Modric, Modric Asisitiza Kuwa Croatia Itakuwa Bora, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa