Georgina Rodriguez amemkosoa meneja wa Ureno Fernando Santos kwenye Instagram kwa uamuzi wake ‘mbaya’ wa kumwanzisha Cristiano Ronaldo kwenye benchi baada ya kuchapo dhidi ya Morocco, huku akisisitiza mpenzi wake ‘alibadilisha’ mchezo ‘lakini ilikuwa muda umeisha’
Mpenzi wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez amemsuta meneja huyo kwa kutomuanzisha mshambuliaji huyo kwenye mchezo wao muhimu na mgumu wa kufuzu hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia.
Ronaldo aliondolewa kwenye kikosi cha kwanza Jumanne wakati Ureno ilipomenyana na Uswizi katika hatua ya 16 bora, na mbadala wake Goncalo Ramos akafunga hat-trick, na kupelekea Santos kumchagua Ramos mbele ya Ronaldo kwa mara nyingine tena dhidi ya Morocco.
Uamuzi huu haukuweza kuzaa matunda kwani Ureno walishindwa kutafuta njia, na wakatupwa nje kufuatia bao la ushindi la Youssef En-Nesyri kipindi cha kwanza. Ronaldo alinyenyuliwa kutoka kwenye benchi kipindi cha pili dakika ya 50, lakini hakuweza kubadilisha mchezo kwa upande wa timu yake, na Rodriguez amemkashifu Santos kwa kutofanya mabadiliko mapema.
Kando ya picha ya Ronaldo, Rodriguez alichapisha kwenye Instagram: “Leo rafiki yako na kocha wameamua vibaya, Rafiki huyo ambaye una maneno mengi ya pongezi na heshima kwake.
“Wala huwezi kushikamana na mtu ambaye hastahili, Maisha hutufundisha masomo. Leo hatujapoteza, tumejifunza.”
Kauli ya Rodriguez inakuja baada ya Santos kusisitiza kuwa hajakosana na Ronaldo, na kudai wawili hao bado wana ‘uhusiano wa karibu sana’ licha ya uamuzi wake wa kumtema mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United.
Rodriguez anaamini Ronaldo hutoa matokeo chanya akitokea benchi, ingawa takwimu za muda wote zinaonyesha kuwa alijitahidi kuingia kwenye mchezo kipindi cha pili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alikuwa na miguso 10 tu mara tu alipoingia, na aliweza kupiga shuti moja tu ambalo lilizuiwa vyema na kipa wa Morocco Yassine Bounou.
Dadake Ronaldo Elma Aveiro pia aliguswa na kichapo hicho, akiwataka wachezaji wa Ureno kuendelea kuinua vichwa vyao baada ya kupoteza.
“Inasikitisha kwa timu, sasa ni wakati wa kuinua vichwa vyetu na kusonga mbele… Mungu anajua kila kitu,” aliandika kwenye Instagram.
Aveiro pia alishiriki chapisho kwenye Instagram yake na hashtag #SantosOut, kwani alionekana kuashiria kuwa ni wakati wa bosi wa Ureno kuacha jukumu lake.
Ronaldo alikuwa akitafuta kushinda Kombe la Dunia baada ya kushiriki kwa mara ya tano bila mafanikio, lakini ameshindwa kwa mara nyingine, na Ureno sasa wameshindwa kufika nusu fainali tangu 2006.
Atakuwa na umri wa miaka 41 wakati Kombe lijalo la Dunia litakapofika, lakini umakini wake sasa unatarajiwa kugeukia pale atakapokuwa akichezea soka la klabu yake, huku fowadi huyo akitafuta timu mpya baada ya kukatishwa mkataba wake United mwezi uliopita.