Mshambuliaji klabu ya Rb Leipzig na timu ya taifa ya Ufaransa Christopher Nkunku ataikosa michuano ya kombe la dunia bgaada ya kupata majeraha akiwa katika kambi ya timu hiyo huko nchini Ufaransa.

Mchezaji huyo ambaye alijumuishwa kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 26 ambacho kitasafiri na timu hiyo leo kuelekea nchini Qatar kwajili ya michuano ya kombe la dunia hivo mchezaji huyo hatakuwemo kwenye timu hiyo.nkunkuMshambuliaji Nkunku ambaye alipata majeraha ya goti siku ya jumanne mazoezini alipogongana na kiungo wa klabu ya Real Madrid wakati wanagombea mpira, Baada ya hapo mshambuliaje huyo alihitaji usaidizi ili kutoka nje ya kiwanja.

Baada ya hapo taarifa ya madaktari kupitia timu ya taifa ya Ufaransa walitoa taarifa ya mshambuliaji huyo kukosekana kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar baada ya kupata majeraha ya goti lake la kushoto.nkunkuNkunku anaikosa michuano ya kombe la dunia ambayo ingekua ya kwanza kwa mchezaji kuitumikia timu ya taifa ya Ufaransa kwenye michuano ya kombe la dunia. Lakini umri wake unamruhusu kama ataendelea kua bora anaweza kuitumikia timu hiyo michuano ijayo ya kombe la dunia mwaka 2026.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa