Gwiji wa Arsenal Ray Parlour amemtaka Gareth Southgate kuwaanzisha wachezaji wawili ambao wapo kwenye kiwango kizuri mpaka sasa ambao ni Ben White wa Arsenal na James Maddison wa Leicester City kwenye mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia dhidi ya Iran.

 

Parlour: Maddison Anafaa Kuanza Mechi ya Kwanza ya Uingereza

Parlour, ambaye alishinda mechi 10 akiwa na Uingereza, alitumia chumba cha kubadilishia nguo na Southgate huko Middlesbrough wakati wa siku zao za kucheza na anaamini kuwa mchezaji mwenzake wa zamani ana maamuzi magumu ya kufanya huko Qatar.

Akizungumza na LiveScore, mtangazaji huyo alichagua safu yake kuelekea mechi hiyo , huku beki wa Gunners, Ben White na mchezaji wa Leicester Maddison wakipigiwa chapuo kubwa la kuanza kwenye mchezo huo.

Parlour: Maddison Anafaa Kuanza Mechi ya Kwanza ya Uingereza

Parlour ambae ana miaka 49, alisema: “Natumai Gareth ataenda na mabeki wanne nyuma dhidi ya Iran. Ningempanga Jordan Pickford katika goli, huku Kieran Trippier na Luke Shaw wakiwa mabeki wa pembeni.”

Aliongezea kwa kusema kuwa; “Kwangu mimi, John Stones lazima acheze katikati, lakini Gareth ana uamuzi mkubwa wa kufanya na nani anayecheza karibu naye.”

Harry Maguire amekuwa na wakati mgumu, na ikiwa hachezi mara kwa mara, ni vigumu kuwa na kasi na uapnde wa ushindani wa mchezo, huku akiendelea kusisitiza kuwa kama angekuwa yeye angecheza kamari kwa kuanza na White.

Parlour: Maddison Anafaa Kuanza Mechi ya Kwanza ya Uingereza

White amekuwa na kipaji kwa Arsenal, mara nyingi akicheza nje ya nafasi lakini hajawahi kuwaangusha kwani mchezaji huyo yupo katika hali nzuri, ana kasi na anategemewa sana katikati ya safu ya ulinzi pia.

Katika safu ya kiungo, nadhani unapaswa kujaribu kumleta Maddison. Tena, ni mchezaji mzuri, mwenye kujiamini na kufunga mabao, pia anasema angewachezesha Declan Rice, Jude Bellingham huku Maddison akiwa mbele yao katika safu ya kiungo.

Parlour: Maddison Anafaa Kuanza Mechi ya Kwanza ya Uingereza

Parlour anasema mbele angemueka Harry Kane, kisha anagemchukua Phil Foden na Bukayo Saka. Kwa upande wa Raheem Sterling amesema hampingi lakini amelinganisha kiwango cha Saka cha hivi karibuni na Raheem, lazima uchague vijana wenye uchu na utulivu kuelekea mechi hizi.

Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Parlour, Parlour: Maddison Anafaa Kuanza Mechi ya Kwanza ya Uingereza, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa