Mchezaji wa klabu ya PSG raia wa Hispania Sergio Ramos ameachwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Hispania kitakachoshiriki michuano ya kombe la dunia mwaka huu yatakayopigwa nchini Qatar mwezi huu.

Kocha wa timu hiyo Luis Enrique ambaye amekitangaza kikosi chake cha wachezaji 26 kitakachoelekea nchini Qatar kwajili ya michuano ya kombe la dunia mwaka huu huku jina la beki huyo wa zamani Real Madrid likiwa halimo.ramosBeki Sergio Ramos ambaye amekua akionesha ubora wa hali ya juu ndani ya PSG lakini kocha huyo amemuacha na kuchukua mabeki wengine ambao inaonekana kama kocha Ramos sio sehemu ya Mipango yake.

Beki huyo mshindi wa kombe la dunia na mataifa ya ulaya na kikosi cha Hispania inakua mara ya pili kuachwa na kwenye kikosi cha Hispania chini ya mwalimu Luis Enrique baada ya kuachwa kwenye kikosi hicho mwaka 2021 kilichoshiriki michuano ya Euro.ramosBaada ya Ramos kuachwa kwenye kikosi cha Hispania imeibua mijadala mingi kutokana na uwezo wake ambao ameuonesha msimu huu ukilinganisha pia na wachezaji wa nafasi yake walioitwa kwenye kikosi hicho.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa