Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Brazil anayekipiga katika klabu ya Tottenham ya nchini Uingereza Richarlison amefunguka na kusema wachezaji wa timu hiyo watapambana kwa kila namna ili kubeba kombe la dunia la sita mwaka huu.

Ikumbukwe Brazil ndio taifa linaloongoza kuchukua kombe hilo huku likiwa tayari limebeba mara tano, Huku likifuatiwa na Italia na Ujerumani kila mmoja akiwa ana makombe mnne jambo hilo ndio limefanya staa huyo kuamini kua wanatakiwa kupambana ili kubeba taji la sita mwaka huu.RicharlisonBrazil tangu wamebeba taji hilo ni miaka takribani 20 sasa imepita kwani mara ya mwisho ilikua mwaka 2002 michuano iliyofanyika Korea na Japani. Richarlison amedai anapenda kufanya kazi yake kwa utulivu na ukimya lakini anaamini Brazil inastahili kushinda kombe la dunia mwaka huu kutokana na ubora wakiokua nao.

Mshambuliaji huyo anasema anaamini kocha wa timu hiyo Tite atawaandaa vizuri kuelekea michuano hiyo ili waweze kufanya vizuri kama ambavyo wamejipanga kwani kila mchezaji ndani ya timu hiyo anatamani kufanya vizuri na timu na kubeba kombe hilo.richarlisonPamoja na hivo Richarlison pia alionelea timu nyingine ambayo anaiona tishio kuelekea michuano hiyo huku akizitaja timu za Ufaransa, Ubelgiji, pamoja na Argentina ambayo iliwafunga kwenye fainali za Copa America.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa