Richarlison Ashinda Bao Bora la Kombe la Dunia

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil anayekipiga katika klabu ya Tottenham Hotspurs ya nchini Uingereza Richarlison ametangazwa kama mshindi wa bao bora la michuano ya kombe la dunia mwaka 2022.

Mchezaji huyo amefanikiwa kutangazwa kama mshindi wa goli bora la michuano ya kombe la dunia kati ya mabao mengi bora yaliyofungwa kwenye michuano hiyo, Bao la mchezaji huyo lililofanikiwa kua bao bora la michuano alifunga katika mchezo wa kwanza wa Brazil dhidi ya timu ya taifa ya Serbia.richarlisonMshambuliaji Richarlison amefanikiwa kuwashinda wachezaji kama Kylian Mbappe, Tchouameni, Goncalo Ramos, pamoja Vicent Aboubakar ambao walikua wanagombani kushinda bao bora la michuano lakini mchezaji huyo akifanikiwa kuibuka mshindi.

Mshambuliaji Richarlison amechukua goli bora akipokea kijiti kwa beki wa Ufaransa Benjamin Pavard ambaye alishinda bao bora la mashindano mwaka 2018 akifunga dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa kwenye hatua ya 16 bora, Lakini mwaka huu goli bora limefungwa kwenye hatua ya makundi.richarlisonPia michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 imefanikiwa kuweka rekodi ya kua michuano iliozalisha mabao mengi zaidi ikifanikiwa kuzalisha mabao 172 ikiipiku kampeni ya mwaka 1998 ambapo yalizalishwa mabao 171.

Acha ujumbe