Gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Fc Barcelona Rivaldo amesema nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi anastahili kubeba kombe la dunia linaloendelea huko nchini Qatar.

Lionel Messi amekua kwenye ubora wa hali ya juu katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la dunia  dhidi ya timu ya taifa ya Croatia baada ya kufanikiwa kufunga bao moja la mkwaju wa penati na kutengeneza mabao mawili kwa kijana mdogo Julian Alvarez.messiKatika michuano hiyo ambayo timu ya taifa ya Argentina ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya timu ya taifa ya Croatia na kufuzu hatua ya fainali ya michuano hiyo, Huku nahodha huyo wa Argentina akifanikiwa kufikisha mabao matano kwenye michuano hiyo.

Staa huyo baada ya kucheza mchezo wa jana amefanikiwa kufikia rekodi ya gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Lothar Mathaus ambaye alicheza michezo 25, Na nahodha huyo wa timu ya taifa ya Argentina akifanikiw kufikisha idadi hiyo ya michezo.messiGwiji wa timu ya taifa ya Brazil na mshindi wa kombe la dunia mwaka 2002 Rivaldo anaeleza kwa wakati huu ambayo Brazil haipo yeye angetamani kuiona Argentina ikibeba kombe la dunia kutokana na ubora ambao Messi ameuonesha kwenye michuano hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa