Sane Kuikosa Mechi ya Ufunguzi ya Ujerumani

Mchezaji wa Bayern Munich na timu ya Taifa ya Ujerumani Leroy Sane atakosa mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia la Ujerumani dhidi ya Japan kutokana na jeraha la goti ambalo amelipata.

 

Sane Kuikosa Mechi ya Ufunguzi ya Ujerumani

Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB) limethibitisha kuwa winga huyo wa Bayern Munich hakuwepo kwenye mazoezi ya mwisho ya Ujerumani ambayo watakuwa  wakijiandaa na mechi ya Kundi E kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Khalifa hapo kesho.

Taarifa ya DFB ilisema: “Timu ya Taifa ya Ujerumani lazima imkose Leroy Sane katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kombe la Dunia dhidi ya Japan siku ya Jumatano. Leroy ambaye ana miaka 26 hatakuwepo kutokana na tatizo la goti.”

Sane Kuikosa Mechi ya Ufunguzi ya Ujerumani

Huku wachezaji 25 ambao walisalia kwenye kikosi cha Ujerumani cha Kombe la Dunia wakishiriki katika mazoezi ya mwisho huko Al-Shamal. Pia wametangaza kuwa baada ya chakula cha mchana, kikosi hicho cha mabingwa mara nne wa Dunia kitaelekea katika mji mkuu wa Qatar, Doha.

Ingawa kumpoteza Sane, ambaye amefunga mara 11 katika mechi 45 alizoichezea nchi yake, ni wazi kuwa ni pigo huku kocha mkuu Hansi Flick akiwa na wachezaji wengi katika nafasi ya ushambuliaji Serge Gnabry, Julian Brandt, Mario Gotze, Kai Havertz na Jamal Musiala.

Sane Kuikosa Mechi ya Ufunguzi ya Ujerumani


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Acha ujumbe