Rais wa zamani wa FIFA Sepp Blatter amedai kuwa ilikuwa ‘kosa’ kukabidhi Kombe la Dunia kwa Qatar kwa sababu ni nchi ‘ndogo’ kuandaa mashindano hayo makubwa.

Utoaji wa Qatar wa shindano hilo la thamani mwaka 2010 ulikabiliwa na utata mkubwa baada ya madai kuwa nchi hiyo ilitoa hongo ili kupata haki ya kuandaa michuano hiyo, huku tarehe ya kuanza kwa mashindano hayo ikibadilishwa hadi msimu wa baridi ili kuepusha wachezaji kushindana katika viwango vya joto.

 

Sepp Blatter: Qatar Haikupwa Kuandaa Kombe la Dunia 2022

Wenyeji hao pia wamekabiliwa na shutuma kutokana na rekodi ya haki za binadamu nchini humo na sheria zake dhidi ya LGBTQ, huku mataifa mengi yakipanga kuweka msimamo dhidi ya ubaguzi watakapowasili Qatar mwezi huu wa Novemba.

Blatter ambaye aliiongoza FIFA kuanzia 1998 hadi 2015 kabla ya kufungiwa kutojihusisha na soka kwa miaka sita kutokana na kashfa ya rushwa, alihojiwa kwa mara ya kwanza tangu kuondolewa mashtaka mwezi Julai.

Alisema ilikuwa ni makosa kuipa Qatar heshima ya uenyeji kutokana na ukubwa wake na kudai kuwa Marekani ndiyo iliyopendekezwa na FIFA kuandaa toleo la 2022 kabla hawajapewa muundo wa 2026.

 

Sepp Blatter: Qatar Haikupwa Kuandaa Kombe la Dunia 2022

“Chaguo la Qatar lilikuwa kosa,” Blatter alikiambia kituo cha Uswizi cha Tages-Anzeiger.

“Wakati huo, tulikubaliana katika kamati kuu kwamba Urusi inapaswa kuandaa Kombe la Dunia la 2018 na USA lile la 2022. Ingekuwa ishara ya amani ikiwa wapinzani wawili wa muda mrefu wa kisiasa wangeandaa Kombe la Dunia mara moja baada ya jingine.

“Ni nchi ndogo sana. Kandanda na Kombe la Dunia ni kubwa mno kwa hilo.”

Alipoulizwa kama alihisi kuwajibika kuipatia Qatar Kombe la Dunia, aliongeza: ‘Kwangu mimi ni wazi: Qatar ni makosa. Chaguo lilikuwa mbaya.

“Ninachojiuliza! kwa nini rais mpya wa Fifa [Gianni Infantino] anaishi Qatar? Hawezi kuwa mkuu wa shirika la ndani la Kombe la Dunia. Hiyo si kazi yake, Kuna kamati mbili za maandalizi ya hili, moja ya ndani na moja kutoka Fifa.”

Mwanzoni mwa mwaka ilidaiwa katika uchunguzi kutoka SonntagsBlick kwamba Infantino alikuwa akiishi Qatar tangu Oktoba 2021, akikodisha nyumba katika mji mkuu wa Doha.

FIFA baadaye ilidai kuwa Infantino anagawanya muda wake kati ya kufanya kazi Doha na Zurich, ambako shirika hilo lina makao yake, na kwamba kuwa Qatar kunamruhusu kuweka umakini wake katika kujiandaa kwa Kombe la Dunia.


Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

AVIATOR

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa