Mchezaji wa Uswizi Xherdan Shaqiri amethibitisha kuwa adui wa Serbia kwa mara nyingine kwa kuwasaidia vijana wa Dragan Stojkovic kwenda 16 bora michuano ya Kombe la Dunia hapo jana kwenye Uwanja wa 974.
Shaqiri alifunga bao la ushindi dakika za mwisho dhidi ya Serbia katika mashindano ya 2018 nchini Urusi na kusherehekea kwa kutengeneza umbo la tai kwa mikono yake kuonyesha kuunga mkono Kosovo, nchi alikozaliwa na jimbo la zamani la Serbia lililojitangazia uhuru mwaka 2008. Uhuru huo haitambuliwi na Serbia.
Mchezaji huyo wa Chicago Fire alizomewa na kukejeliwa wakati shabiki mmoja wa Serbia alitupwa nje kwa kuimba dhidi ya Kosovo, huku mchezaji huyo alifurahia kwa kufunga bao la kwanza kwa Uswizi ambao waliingia kwenye mchezo huo wakijua sare ingewatosha.
Uswizi walisonga mbele kutoka Kundi G kwa ushindi wa 3-2, pamoja na Brazil licha ya kushindwa kwao 1-0 na Cameroon.
Shaqiri na Taifa lake la Uswizi watacheza hatua ya 16 bora siku ya Jumanne dhidi ya Ureno huku kila mmoja akiuhitaji ushindi huo ambao utafanya aende hatua ya robo fainali.