Timu ya taifa ya Ufaransa chini ya kocha Didier Deschamps imeongeza mchezaji mmoja kwenye kikosi chake na kutimiza wachezaji 26 baada ya hapo awali kuita wachezaji 25 sasa wako tayari kuelekea Qatar.
Mabingwa hao watetezi wa michuano hiyo wametimiza orodha ya wachezaji 26 baada ya kumjumuisha mtoto wa gwiji wa zamani wa taifa hilo Lilian Thuram aanayecheza ligi kuu ya Ujerumani katika klabu ya Borussia Monchengladbach anayefahamika kama Marcus Thuram.Marcus Thuram ambae anacheza nafasi ya ushambuliaji anakwenda kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya taifa hilo inayoongezwa na Karim Benzema, Kylian Mbappe, pamoja Olivier Giroud.
Kikosi cha Ufaransa ni miongoni vikosi vinavyopewa nafasi ya kubeba ubingwa wa kombe la dunia nchini Qatar kwasababu ya vipaji ambavyo imejumuisha kwenye kikosi chake kuanzia safu ya ulinzi, katikati ya kiwanja na eneo la ushambuliaji.Ufaransa wanaenda kwenye kombe dunia bila baadhi ya wachezaji wake muhimu ambao walicheza kwa kiwango kikubwa wakati timu hiyo inashinda kombe la dunia 2018 kama Paul Pogba na Ngolo Kante.